UTENZI:NAKULILIA MAGUFULI
1.
Mwangaza umeshazima
Nchiyo inazizima
Vitu vyote mesimama
Tumebaki ka yatima.
2.
Flayova alijenga
Mishahara bila chenga
Wananchi walilonga
Shida zao kaziganga.
3.
Miji yote iling'aa
Kwa umeme kusambaa
Kila kona ya mtaa
Magufuli aliweka.
4.
Elimu bure shuleni
Wanafunzi kasomeni
Madawati darasani
Magufuli alipania.
5.
Bodaboda barabara
Zimejengwa kwa imara
Mutembee kwa busara
Magufuli alijenga.
6.
Ni kilio kwa hakika
Nchi imetikisika
Machozi yanatutoka
Magufuli kaondoka.
7
Imekuwa ni mapema
Kuondoka ulo mwema
Ulale mahali pema
Raisi wetu magufuli.
8.
Watumishi uliahidi
Neema kuzifaidi
Mapato yatapozidi
Hakika ulipania.
9.
Uchungu menilemea
Mbele sitoendelea
Machozi yamenijia
Magufuli nakulilia.
Itaendelea........
Utenzi umeandikwa na
Mwl Godoni Y Bayalimo
Mnamo tar 21.03.2021 kufuatia kifo cha aliyekuwa raisi wa Tanzania kilichotokea tar 17.03.2021.
Comments
Kwa umahili hakika
Menivutia sana
Kwayo mawaidha
Pongezi pokea
Wala sipuuzie.
������������.
Dogo uko vizuri sana