Posts

Showing posts from February 22, 2020

Tujumuikeni by mwl Godoni Yohana.

Image
POEM NO 9 Nawasalimu washairi Mlojazwa umahiri Karibuni medanini Tuyatoe ya moyoni Yaletayo ahueni Kwa wanyonge, Tujumuikeni. Alo mbele ni Jaalali Vikwazo viwe mbali Tumsifu kwa morali Tujumuikeni. Nambari ilo ya pili Tuwasifu wenye mimbari Ya ushairi na tunzo Watunzi tutunzweni, Tujumuikeni. Ni tungo zilo huru Nipendazo  hadi leo Zisopuuza mapokeo Wanaasili jasiri Mujumuikeni. Karibuni e hadhira Sataranjini pa kukaa Mlikaribie jukwaa La malenga wa Tanzania Tujumuikeni. Mola tutabaruku Sime tuishike Tukimbize ubaramaki Taji watuvike Tujumuikeni. Walianza enzi zile Malenga walo wa kweli Wakapanda mbegu zile Za ushairi ni mali Washairi Tujumuikeni. Adili zao walitoa Kwa watoto na vijana Watu wote wakasikia Na hata wazee pia Tujumuikeni.