Posts

Showing posts from February 19, 2020

Mu wapi malenga? by Godoni Yohana.

POEM NO 8 Kichwa changu chanigonga Kikiwasaka malenga Malenga waliojipanga Kukipuliza kipenga Kipenga cha waganga Watulizao yugayuga. Mu wapi malenga Tuyaanze majibizano? Nawasaka kama nini Muje medanini Kaskazi hadi kusini Njooni musinihini Ushairi tuuthamini Wala tusiuhini. Mu wapi malenga Tuyaanze majibizano? Ushairi kwangu lulu Kwako nakuwaje, Hunipatia uhuru Nawe waonaje Ñaipaisha Kasulu Wewe unafanyaje?. Mu wapi malenga Tuyaanze majibizano? Tamati nimefikia Ya shairi kuandika Upweke ulinizidia Pekee kusikika Nkaamua kuwajia Mkekani kuwaalika Mu wapi malenga Tuyaanze majibizano?.