Mu wapi malenga? by Godoni Yohana.

POEM NO 8

Kichwa changu chanigonga
Kikiwasaka malenga
Malenga waliojipanga
Kukipuliza kipenga
Kipenga cha waganga
Watulizao yugayuga.
Mu wapi malenga
Tuyaanze majibizano?

Nawasaka kama nini
Muje medanini
Kaskazi hadi kusini
Njooni musinihini
Ushairi tuuthamini
Wala tusiuhini.
Mu wapi malenga
Tuyaanze majibizano?

Ushairi kwangu lulu
Kwako nakuwaje,
Hunipatia uhuru
Nawe waonaje
Ñaipaisha Kasulu
Wewe unafanyaje?.
Mu wapi malenga
Tuyaanze majibizano?

Tamati nimefikia
Ya shairi kuandika
Upweke ulinizidia
Pekee kusikika
Nkaamua kuwajia
Mkekani kuwaalika
Mu wapi malenga
Tuyaanze majibizano?.

Comments

Popular posts from this blog

UTENZI:NAKULILIA MAGUFULI

UNTOUCH YOUR FATHER'S BEARDS by mwl Godoni Yohana