Posts

Showing posts from March 21, 2021

UTENZI:NAKULILIA MAGUFULI

Image
POEM NO 16 POEM NO 16  1. Mwangaza umeshazima Nchiyo inazizima Vitu vyote mesimama Tumebaki ka yatima. 2. Flayova alijenga Mishahara bila chenga Wananchi walilonga Shida zao kaziganga. 3. Miji yote iling'aa Kwa umeme kusambaa Kila kona ya mtaa Magufuli aliweka. 4. Elimu bure shuleni Wanafunzi kasomeni Madawati darasani Magufuli alipania. 5. Bodaboda barabara Zimejengwa kwa imara Mutembee kwa busara Magufuli alijenga. 6. Ni kilio kwa hakika Nchi imetikisika Machozi yanatutoka Magufuli kaondoka. 7 Imekuwa ni mapema Kuondoka ulo mwema Ulale mahali pema Raisi wetu magufuli. 8. Watumishi uliahidi Neema kuzifaidi Mapato yatapozidi Hakika ulipania. 9. Uchungu menilemea Mbele sitoendelea Machozi yamenijia Magufuli nakulilia. Itaendelea........ Utenzi umeandikwa na  Mwl Godoni Y Bayalimo Mnamo tar 21.03.2021 kufuatia kifo cha aliyekuwa raisi wa Tanzania kilichotokea tar 17.03.2021.