Tujumuikeni by mwl Godoni Yohana.
POEM NO 9
Nawasalimu washairi
Mlojazwa umahiri
Karibuni medanini
Tuyatoe ya moyoni
Yaletayo ahueni
Kwa wanyonge,
Tujumuikeni.
Alo mbele ni Jaalali
Vikwazo viwe mbali
Tumsifu kwa morali
Tujumuikeni.
Nambari ilo ya pili
Tuwasifu wenye mimbari
Ya ushairi na tunzo
Watunzi tutunzweni,
Tujumuikeni.
Ni tungo zilo huru
Nipendazo hadi leo
Zisopuuza mapokeo
Wanaasili jasiri
Mujumuikeni.
Karibuni e hadhira
Sataranjini pa kukaa
Mlikaribie jukwaa
La malenga wa Tanzania
Tujumuikeni.
Mola tutabaruku
Sime tuishike
Tukimbize ubaramaki
Taji watuvike
Tujumuikeni.
Walianza enzi zile
Malenga walo wa kweli
Wakapanda mbegu zile
Za ushairi ni mali
Washairi
Tujumuikeni.
Adili zao walitoa
Kwa watoto na vijana
Watu wote wakasikia
Na hata wazee pia
Tujumuikeni.
Nawasalimu washairi
Mlojazwa umahiri
Karibuni medanini
Tuyatoe ya moyoni
Yaletayo ahueni
Kwa wanyonge,
Tujumuikeni.
Alo mbele ni Jaalali
Vikwazo viwe mbali
Tumsifu kwa morali
Tujumuikeni.
Nambari ilo ya pili
Tuwasifu wenye mimbari
Ya ushairi na tunzo
Watunzi tutunzweni,
Tujumuikeni.
Ni tungo zilo huru
Nipendazo hadi leo
Zisopuuza mapokeo
Wanaasili jasiri
Mujumuikeni.
Karibuni e hadhira
Sataranjini pa kukaa
Mlikaribie jukwaa
La malenga wa Tanzania
Tujumuikeni.
Mola tutabaruku
Sime tuishike
Tukimbize ubaramaki
Taji watuvike
Tujumuikeni.
Walianza enzi zile
Malenga walo wa kweli
Wakapanda mbegu zile
Za ushairi ni mali
Washairi
Tujumuikeni.
Adili zao walitoa
Kwa watoto na vijana
Watu wote wakasikia
Na hata wazee pia
Tujumuikeni.
Comments